#HABARI: Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Mhe. Dkt. Emmanuel Nuwas, ameadhimisha Sikukuu ya Krismasi kwa namna ya kipekee kwa kushiriki hafla ya chakula cha mchana na watu wenye ulemavu jimboni humo. Katika hafla hiyo, Mheshimiwa Mbunge alitoa misaada mbalimbali ya kibinadamu ikiwa ni ishara ya upendo na mshikamano, akilenga kuwawezesha walengwa kusherehekea msimu huu wa sikukuu kwa furaha na faraja.
Lengo kuu la tukio hilo lilikuwa ni kuhakikisha kuwa kila mwananchi, bila kujali hali yake, anapata fursa ya kufurahia baraka za Krismasi katika hali ya amani na utulivu. Kitendo hiki cha kutoa misaada kimepokelewa kwa shukrani kubwa, kikionyesha umuhimu wa viongozi kuwa karibu na jamii na kuwajali wenye uhitaji katika msimu huu wa kumshukuru Mungu na kupeana kheri.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.