
Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Gideon Saar, amesema serikali za kigeni hazina haki ya kuwazuia Wayahudi kuishi katika kile alichokiita Ardhi ya Israel, akitaja ukosoaji huo kuwa unawabagua Wayahudi.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametangaza kuwa nchi hiyo inapanga kuwekeza dola bilioni 110 katika kipindi cha miaka kumi ijayo ili kuimarisha sekta ya ndani ya utengenezaji wa silaha. Akizungumza katika hafla ya mahafali ya marubani wapya wa jeshi la anga, Netanyahu amesema mpango huo unalenga kupunguza utegemezi wa Israel kwa wauzaji wa silaha wa nje, akibainisha kuwa hata mataifa rafiki, yakiwemo Ujerumani, yataongeza ununuzi wa silaha kutoka Israel.