SIKUKUU ya Krismasi imeendelea kuwa chanzo cha fursa kwa wananchi, hususan wale wanaojishughulisha na huduma katika maeneo ya burudani. Wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam, mpigapicha maarufu anayejulikana kama Rasta amesema sikukuu hiyo imemfungulia fursa ya kuongeza kipato tofauti na siku za kawaida.

Akizungumza akiwa kazini katika moja ya fukwe za jiji hilo, Rasta alisema kwa siku za kawaida hutoza Sh 2,000 kwa picha moja isiyohaririwa na Sh 3,000 kwa picha iliyohaririwa (filtered). Hata hivyo, leo Desemba 25 hali imekuwa tofauti kutokana na ongezeko la wateja, jambo lililomfanya kupandisha bei hadi kati ya Sh 3,000 na Sh 4,000 kwa picha moja.

Amesema pamoja na kupanda kwa bei, idadi ya watu wanaohitaji huduma ya upigaji picha imeongezeka kwa kiasi kikubwa kutokana na wakazi wengi wa jiji kujitokeza kusherehekea sikukuu katika fukwe mbalimbali.  Mbali na upigaji picha, fursa nyingine zilizoonekana kunawiri ni pamoja na ukodishaji wa maboya ya kuogelea na uuzaji wa barafu tamu (ice cream), ambavyo vimekuwa vikiwavutia watoto na watu wazima.

Kwa muda mrefu, imekuwa desturi kwa wakazi wa Dar es Salaam kutumia fukwe kama maeneo ya kupumzika na kufurahia sikukuu, jambo linaloendelea kuchochea shughuli ndogondogo za kiuchumi kwa wananchi. SOMA: Wazazi waaswa kuangalia watoto Ufukweni

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *