p

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 4

Arsenal watakuwa wanaongoza Ligi Kuu England wakati wa Krismasi kwa mara ya tatu katika kipindi cha miaka minne baada ya ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Everton, kumaanisha kuwa wamewapita Manchester City.

Kwa ujumla ni mara ya tano kwa Arsenal kuongoza Ligi Kuu siku ya Krismasi, kwa bahati mbaya mara nne zilizopita wameshindwa kutwaa Kombe la Ligi Kuu England mwishoni mwa msimu.

Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2002/03 ambapo Arsenal, waliongoza ligi wakati wa Krismasi lakini wakashindwa kutwaa taji na likabebwa na Manchester United. Kisha mwaka 2007/08 waliongoza jedwali wakati wa Krismasi lakini wakamaliza katika nafasi ya tatu, huku Man Utd wakiwa mabingwa tena.

Ukijumlisha na mwaka huu, chini ya meneja wa sasa Mikel Arteta, wamekuwa kileleni mara tatu wakati wa Siku ya Krismasi kutoka 2022/23 na 2023/24, lakini kila mara walizidiwa na Man City, wapinzani wao wa karibu msimu huu, wakiwa nyuma kwa pointi mbili.

Gunners walikuwa mbele kwa pointi sita dhidi ya Man City siku ya Krismasi 2023 lakini hatimaye walimaliza wakiwa nyuma kwa pointi mbili mwezi Mei.

Pia unaweza kusoma

Ushindi na Krismasi

l

Chanzo cha picha, Getty Images

Historia inaonyesha zaidi ya nusu ya timu zinazoongoza jadweli wakati wa Krismasi hushinda taji la Ligi Kuu.

Katika misimu 17 kati ya 33 ya Ligi Kuu hadi sasa, timu iliyoketi kileleni Desemba 25 iliendelea mbele na kutwaa kombe, lakini katika misimu mingine 16 walikosa.

Mara nne za mwisho ambapo timu inayoongoza wakati wa Krismasi imeshindwa na Man City ambao hutoka nyuma na kutawazwa mabingwa.

Walikuwa pointi nane nyuma ya Liverpool katika msimu wa 2020/21, pointi nne nyuma ya Liverpool katika msimu wa 2022/23 na pointi sita nyuma ya Arsenal katika nafasi ya tano katika msimu wa 2023/24.

Kupanda kwa Man City kutoka nafasi ya tano mwaka 2023/24 kulifanya kuwa mara ya nne kwa timu ya nje ya nne bora siku ya Krismasi kutawazwa mabingwa mwishoni mwa msimu.

Time tatu zilizofanya kama hivyo ni Man Utd, ambao walikuwa wa tano msimu wa 1996/97, Arsenal (wa sita msimu wa 1997/98) na City (wa nane msimu wa 2020/21).

Rekodi ya kuwa na pointi nyingi nyuma wakati wa Krismasi kabla ya kushinda taji la Ligi Kuu ni ya Arsenal, ambao walikuwa nyuma kwa pointi 13 dhidi ya Man Utd 1997/98.

Kushuka Daraja na Krismasi

d

Chanzo cha picha, Ron Sports

Timu tatu za mwisho wakati wa Krimasi zitakuwa ni Wolverhampton Wanderers, Burnley na West Ham. Wolves walikuwa katika nafasi hii msimu uliopita, pamoja na Ipswich Town na Southampton, ingawa walikuwa na pointi nyingi zaidi kuliko sasa.

Ni mara nne pekee ambapo timu tatu za mwisho wakati wa Krismasi zilishuka daraja mwishoni mwa msimu: 2001/02 – Derby County, Leicester City, Ipswich; 2012/13 – Wigan Athletic, Queens Park Rangers, Reading; 2020/21 – Fulham, West Bromwich Albion, Sheffield United; 2023/24 – Luton Town, Burnley na Sheff Utd.

Ni mara nne kwa timu iliyo chini kabisa Siku ya Krismasi imeweza kubaki kwenye ligi: 2004/05 – West Brom; 2013/14 – Sunderland; 2014/15 – Leicester; 2022/23 – Wolves.

Na timu mbili zilizokuwa katika 10 bora Desemba 25 zimeanguka na kushushwa daraja mwisho wa msimu. Blackpool ilishuka daraja licha ya kuwa ya 10 msimu wa 2010/11. Na hata timu iliyo katika nafasi ya saba, iliwahi kuanguka hadi kufikia kiwango cha kushushwa daraja – nayo ni Norwich City mnamo 1994/95.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *