Michuano ya Kombe la Mataifa barani AfrikaAFCON 2025, imeendelea kutimua vumbi nchini Morocco. Usiku wa kuamkia leo Cameroon walipata ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya Gabon.

Katika mchezo wa awali kabisa hapo jana Jumatano Algeria waliitandika Sudan 3-0 huku mabingwa watetezi wa michuano hiyo Ivory Coast wakiwazaba Msumbiji 1-0.

Mechi hizo zimekamilisha mzunguko wa kwanza kwa kila timu na sasa zinasubiriwa mechi za mzunguko wa pili zinazotarajiwa kuanza hapo kesho.

Misri watacheza na Afrika ya Kusini mapema kabisa, Zambia watafuatia dhidi yaComoro huku mechi ya usiku ikiwa ni kati ya wenyeji Morocco dhidi ya Mali. 
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *