Dunia inaadhimisha sikukuu ya Krismasi Alhamisi Desemba 25, siku ambayo Wakiristo wanakumbuka kuzaliwa kwa Mwokozi Yesu Kristo, ambapo ibada zinafanyika Makanisani, huku wengine wakisherehekea  majumbani na katika maeneo mengine ya starehe.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika huku baadhi ya mataifa kama Sudan na Ukraine yakiendelea kukabiliwa na vita.

Kwa mara ya kwanza, sikiuuu ya Krismasi inaadhimishwa kwenye mji wa Bethlhem, uliopo kwenye mamlaka ya Palestina,  inakoaminiwa alizaliwa Yesu Kristo.

Sherehe za mwaka huu zinafanyika baada ya kupatikana kwa mkataba wa kusitisha vita kati ya kundi la Hamas na Israel miezi kadhaa iliyopita.

Katika mkesha wa wa Krismasi siku ya Jumatano, mamia ya wauamini wa Kikiristo walifurika katika Kanisa kuu  mji wa Bethlehem, kwa ajili ya maadhimisho hayo.

Papa Leo wa XIV wakati wa mkesha wa Krismasi, mjini Vatican Desemba 24 2025.
Papa Leo wa XIV wakati wa mkesha wa Krismasi, mjini Vatican Desemba 24 2025. © Gregorio Borgia / AP

Mjini Vatican, kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Leo wa Kumi na sita, anaongoza  misa ya Krismasi yake ya  kwanza baada ya kushika nafasi hiyo.

Katika ujumbe wake wakati wa mkesha wa sikukuu hii, kiongozi huyo ametoa wito wa kuwepo kwa amani kote duniani, hasa katika saa 24 za maadhimisho ya Krismasi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *