Tofauti na mtangulizi wake, Papa Leo alianza kuadhimisha ibada ya mkesho muda mchache kuelekea saa sita usiku, huku akiendesha ibada hiyo kwa muda mrefu.

Baadhi ya vyombo vya habari vimechukulia hatua hiyo kama marejeo ya desturi za zamani za kanisa hilo.

Siku ya Alhamisi, ambayo ndiyo Krismasi yenyewe, Baba Mtakatifu atawasilisha ujumbe maarufu wa “Urbi et Orbi”, ambao utaangazia mambo mbalimbali ulimwenguni.

Papa Leo wa 14, ambaye jina lake halisi ni Robert Francis Prevost alichaguliwa Mei 8, 2025 kama kiongozi wa 267 wa Kanisa Katoliki duniani, kufuatia kifo cha Papa Francis kilichotokea Aprili 21, 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *