
Kiongozi wa Kanisa Kuu Katoliki Duniani Papa Leo XIVametoa wito wa huruma na amani duniani katika misa yake ya kwanza ya Krismasi mjini Roma siku ya Jumatano.
Papa Leo amekumbusha kwamba sikukuu yaKrismasini ya matumaini na inawakumbusha watu kuwa wajumbe wa amani na kwamba utu wa binadamu hauna kikomo.
Katika misa hiyo, Papa huyo mzaliwa wa Marekani ameombea kupatikana kwa amani katika mizozo yote inayoendelea duniani ikiwemo vita vya Urusi nchini Ukraine na pia ameelezea kuhusu hali huko mashariki ya kati.
Kiongozi huyo wa kiroho ambaye alianza kuhudumu mwezi Mei, ataongoza hii leo misa kuu katikaKanisa Kuu la Mtakatifu Petro, ambako anatarajiwa kulaani vita na vurugu na kukumbusha kuhusu mateso ya raia.