
Klabu ya TMA Stars FC kupitia kwa Katibu wake Mkuu, Mbwana Hamad Mbwana umetangaza kusitisha mkataba na aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Habibu Kondo pamoja na wasaidizi wake.
Kupitia taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imesema sababu za kusitisha mikataba yao ni kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo inayoshiriki Ligi ya Championship.
“Klabu ya TMA Stars FC inatangaza kusitisha mkataba na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Timu Bw: Habibu Kondo. Aidha klabu imefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na aliyekuwa Kocha Msaidizi Bw: Agustino Thomas, Kocha wa Magolikipa Bw: Ally Mustafa na Kocha wa Viungo Bw: Kigi Makasi kuanzia tarehe 24/12/2025”.
“Klabu imefikia hatua hii kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa timu kwenye Ligi ya Championship”
“Klabu inawatakia kila la kheri katika majukumu yao mapya”.
Hadi sasa TMA katika ligi ya Championship ipo nafasi ya 11 kati ya timu 16 zinazoshiriki ikivuna pointi 12, imeshinda mechi tatu, droo tatu na kupoteza mechi tano.