Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema yuko tayari kuondoa wanajeshi wake katika mji wa Donbas ambao ni kitovu cha viwanda mashariki mwa nchi hiyo kama sehemu ya mpango wa kumaliza vita vyake na Urusi lakini kwa sharti kwamba Urusi nayo ijiondoe katika eneo hilo na liwekwe chini ya uangalizi wa vikosi vya kimataifa.

Tamko hilo la Zelenskyy linakuja baada ya pendekezo laMarekani la kuundwa kwa “eneo huria la kiuchumi,”. Lakini hata hivyo, kiongozi huyo hakuweka wazi juu ya hatma ya mipango ya kiutawala au maendeleo ya eneo hilo.

Urusi kwa upande wake haijatoa tamko lolote ikiwa itakubali kujiondoa katika maeneo ambayo tayari imeyanyakua nchini Ukraine.

Marekani ambayo nimpatanishiwa mzozo huo imekuwa ikipambana kutafuta suluhu baina ya nchi hizo mbili lakini bila mafanikio mpaka sasa.
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *