Utawala wa Trump unapanga kununua maghala ya kuwahifadhi wahamiaji wasio na vibali. Mpango unaojadiliwa unalenga kuharakisha kukamatwa na kufukuzwa kwa wahamiaji nchini, ambao umeongezeka tangu Donald Trump arejee madarakani.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini New York, Loubna Anaki

Taarifa hiyo imefichuliwa na vyombo vya habari vya Marekani, ambavyo vinadai kupata hati za ndani kutoka ICE, mamlaka ya uhamiaji. Utawala wa Trump unaripotiwa kuwa katika mazungumzo ya kununua maghala saba, ambayo kwa kawaida ni ya kampuni kubwa za usafirishaji na usambazaji bodhaa, lakini ambayo yangebadilishwa kuwa vituo vya kuzuiliwa kwa wahamiaji.

Maghala haya mara mbili ya ukubwa wa vituo vilivyojaa watu kwa sasa, yanatarajiwa kuwahifadhi karibu watu 80,000 wanaosubiri kufukuzwa nchini. Utawala wa Trump unatumai hii itawezesha kuharakisha sera yake ya kupambana na uhamiaji.

Vituo wanakozuiliwa watu vyenye hali “isiyo ya kibinadamu”

Tangu kurejea madarakani kwa Donald Trump mapema mwaka wa 2025, Wizara ya Usalama wa Nchi, ambayo inasimamia shughuli hizi, imetekeleza mbinu zenye utata mkubwa. Vituo wanakozuiliwa watu mara nyingi hukosolewa kwa mazingira yao, yanayoelezewa na mashirika mengi kama “magumu” au hata “yasiyo ya kibinadamu”.

Wahamiaji kadhaa wamefariki wakati wa kizuizini chao. Licha ya ukosoaji huo, mamlaka ya Marekani bado imeazimia kuendelea na vitendo vyake dhidi ya wageni. Hii ilikuwa ahadi ya kampeni ya rais Donald Trump.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *