WAUMINI katika makanisa mbalimbali Zanzibar wametakiwa kuenzi upendo, amani na maadili mema katika maisha yao ya kila siku kama maana halisi ya Krismasi. Ibada za Krismasi zimeendelea kutoka usiku wa December 24 hadi asubuhi ya December 25, zikijumuisha Misa ya Alfajiri na sala maalum zilizoambatana na nyimbo za shukrani na maombi ya kipekee.

Akitoa ujumbe katika Kanisa Katoliki la Minara Miwili, Katibu wa Askofu wa Jimbo la Zanzibar, Father Mapendo Onex, amewaonya waumini kuwa jamii inayokiuka amri za Mungu inaweza kuingia katika hali za kutokuwepo amani, ukosefu wa mshikamano na ubaguzi. “Weka Mungu katikati ya mioyo yenu; hili litakuza upendo, kuimarisha amani na kukuza maisha yenye furaha kwa pamoja.”

Vilevile, katika Kanisa la Anglican Mkunazini, Father Nuoh Salanya amebainisha kuwa  changamoto zinazokumba jamii kama vile vurugu, matumizi ya dawa za kulevya na utapeli, akisisitiza kuwa kuzaliwa kwa Yesu Kristi kunabeba ujumbe wa matumaini mapya. SOMA: Rais Samia:Krismasi itukumbushe upendo

Amewahimiza waumini kuimarisha imani yao, kuepuka matendo yanayoharibu heshima ya binadamu, na kutumia mafundisho ya Kikristo kama mwongozo wa maisha ya kila siku. Alisema: “Tuchukue msimu huu kuendeleza upendo, kuishi kwa amani, na kufuata mafundisho ya Yesu kuhusu uvumilivu, msamaha na utunzaji wa masikini.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *