Kazem Gharibabadi Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Anayehusika na Masuala ya Kisheria na Kimataifa ameissitiza kuwa mashambulizi ya adui dhidi ya raia na makazi ya watu wakati wa vita haramu vilivyoanzisha na Marekani kwa kushrikiana na Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mwezi Juni mwaka huu yamethibitisha kuwa kadhia ya nyuklia ilikuwa kisingiizo tu cha kuishambulia nchi hii.

Gharibabadi amesema kuwa uadui dhidi ya Iran hautokani na mpango wake wa nyuklia, bali unatokana na kwa kuwa nchi ya Kiislamu, kuwa huru na maendeleo yake.

Amesisitiza kuwa uadui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ulitokana na kupingwa misingi hii tajwa badala ya mzozo wowote wa kiufundi au wa kidiplomasia kuhusu faili la nyuklia.

Gharibabadi ameashiria mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na serikali ya Marekani kabla ya vita na kusema mazungumzo hayo yalikuwa yakiendelea kwa kutoiamini kikamilifu Washington na huku kukiwa na kujiandaa kikamilifu kukabiliana na hatua zozote tarajiwa za kijeshi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Anayehusika na Masuala ya Kisheria na Kimataifa amesema: Maadui walikuwa wamejitayarisha kwa uchokozi kwa miaka mingi.

Amesema: Vita vya Israel na Marekani mbali na kuwashambulia raia na makazi ya watu, vililenga pia miundombinu mbalimbali ya Iran. 

“Utawala wa Israel na Marekani ziligonga mwamba kikamilifu katika hatua zao za kijeshi na kushindwa kufanikisha malengo yao ya kimkakati,” amesema Kazem Gharibabadi. 

Mwanadilplomasia huyo wa Iran amesema, badala yake, Jamhuri ya Kiislamu ilitoa vichapo na  maumivu makali kwa utawala huo hadi ukalazimika kusimamisha vita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *