
Kampeni za uchaguzi wa urais uliyopangwa kufanyika siku ya Jumapili, Desemba 28, zimemalizika siku ya Alhamisi jioni, Desemba 25. Siku mbili za kutokuwa na harakati zozote za kisiasa lazima sasa zizingatiwe. Wagombea tisa walifanya mikutano yao ya mwisho, hasa Conakry, baada ya kutembelea maeneo ya ndani ya nchi. Kampeni hii, tofauti na ile iliyopita, haikuvutia umati mkubwa wa watu. Vikwazo vilionekana sana kuwa vya chini, kutokana na kutokuwepo kwa vigogo wa upinzani.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Conakry, Tangi Bihan
Huko Conakry, mji mkuu wa Guinea, ili kuhitimisha kampeni ya kambi yake, Mamadi Doumbouya alishirikiana na wafuasi wake, waliokusanyika kwenye ukumbi wa makao makuu ya Bunge wakiwa na picha kubwa za kiongozi wao wakionekana kucheza muziki. Lakini hakusema neno lolote. Akitafuta kuchaguliwa tena, Mamady Doumbouya hakutoa hotuba za umma, akipendelea kuwaacha mawaziri wake wafanye kampeni kwa niaba yake katika miji mbalimbali kote nchini.
Wagombea wengine, kama vile Abdoulaye Yéro Baldé na Faya Millimouno, walifanya mikutano yao ya mwisho katika vitongoji vya mji mkuu, baada ya kuzunguka nchi nzima kujaribu kuwashwishi wapiga kura waweze kuwapigia kura.
Kazi hii ilizidi kuwa ngumu kutokana na kwamba vyama vya rais wa zamani Alpha Condé na Cellou Dalein Diallo vilikataa kuidhinisha mgombea mmoja ili waweze kumuunga mkono. “Kutokuwepo kwao kuliathiri mengi; hakukuwa na shauku wakati wa kampeni hii,” amesema mtoa maoni mmoja wa kisiasa.
Wiki hii ya mwisho ya kampeni pia ilishuhudiwa na kufungwa kwa baadhi ya majukwaa ya mitandao ya kijamii. Tangu siku ya Jumatatu, imekuwa vigumu kuwasiliana bila kutumia VPN. Na katika mji mkuu, idadi ya vikosi vya usalama, ambayo tayari ni kubwa, imeongzewa zaidi.