
Baada ya zaidi ya miaka miwili ya vita, Hospitali ya Al-Awda katika wilaya ya Nuseirat, katikati ya Gaza, inahudumia takriban wagonjwa 60 waliolazwa na kupokea karibu watu 1,000 wanaotafuta matibabu kila siku Ahmed Mehanna, afisa mwandamizi anayehusika na usimamizi wa hospitali hiyo anasema huduma nyingi zimesitishwa kwa muda kutokana na uhaba wa mafuta yanayohitajika kwa jenereta, na kwamba idara muhimu pekee ndizo zinazoendelea kufanya kazi: kitengo cha dharura, wodi ya uzazi na idara ya watoto.Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali ni kwamba licha ya usitishaji mapigano dhaifu unaoendelea tangu Oktoba 10, bado Ukanda wa Gaza unakabiliwa na mgogoro mkali wa kibinadamu. Wakati makubaliano ya kusitisha mapigano yalibainisha kuingia kwa malori 600 ya misaada kwa siku Gaza, kwa sasa ni malori 100 hadi 300 pekee yanayobeba misaada ya kibinadamu yanayoweza kuingia.