itvtz

#HABARI: Serikali imeagiza kufanyika kwa uchunguzi wa kina katika Hospitali ya Temeke kufuatia kubainika kwa utendaji usioridhisha na vitendo vya rushwa, uzembe na ukosefu wa maadili miongoni mwa baadhi ya watumishi wa hospitali hiyo.

‎Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, John Mapepele, Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amepokea taarifa za malalamiko kuhusu kuzimwa kwa Mashine ya X-Ray na tuhuma za rushwa zinazohusisha baadhi ya walinzi na watoa huduma.

‎Katika uchunguzi wa awali uliofanywa kwa siri na Waziri Mchengerwa, imebainika kuwa baadhi ya walinzi na watumishi wamekuwa wakihusishwa na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa, kutoa lugha zisizofaa kwa wagonjwa, na kuwanyanyasa wateja kinyume na maadili ya kazi.

‎Kufuatia hali hiyo, Waziri Mchengerwa amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe, kufanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha changamoto hizo na kuchukua hatua za kinidhamu kwa watakaobainika kuhusika.

‎Aidha, Waziri huyo ametoa wito kwa watumishi wote wa sekta ya afya kubadilika na kufanya kazi kwa weledi, akisisitiza kuwa Serikali haitavumilia uzembe, rushwa, au ukiukwaji wa maadili ya utumishi wa umma.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *