k

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 4

Vyombo vya habari vya Israel vimekuwa vikichapisha ripoti katika siku za hivi karibuni kuhusu hatari ya makombora ya Iran. Yaani juhudi za Jamhuri ya Kiislamu za kujenga upya uwezo wake wa makombora.

Haya yanajiri huku Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akipanga kusafiri kwenda Marekani katika siku chache zijazo ili kukutana na Rais wa Marekani.

Inaripotiwa kuwa Waziri Mkuu wa Israel anatafuta idhini ya Donald Trump ili kuishambulia Iran tena.

Pia unaweza kusoma

Makombora ya Iran

k

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati wa vita vya siku 12, kipaumbele kilikuwa ni kushambulia vituo vya nyuklia na watu binafsi wanaohusishwa na programu za kijeshi za Iran, pia kulikuwa na mashambulizi mengi dhidi ya taasisi za utafiti, maabara, viwanda, pamoja na maeneo ya kurusha makombora na vituo vya makombora vya Iran.

Kulingana na Hamidreza Azizi, mtaalamu wa Mashariki ya Kati, mashambulizi ya Israel hayakuathiri pakubwa uwezo wa makombora wa Iran.

“Hakuna ripoti za kuaminika kwamba makombora ya Iran yaliharibiwa wakati wa vita vya siku 12. Mjadala pekee ulikuwa kuhusu maeneo ya kurusha makombora na milango ya kuingia na kutokea kwenye kambi za makombora za Iran.”

Kwa maneno mengine, mashambulizi hayo yalikuwa na athari ndogo kwenye makombora, yalilenga zaidi kuharibu maeneo na vifaa vinavyotumika kuhifadhi au kupakia makombora.

Mtaalamu huyo wa masuala ya kijeshi pia anaamini, kwa kuwa makombora mengi yamehifadhiwa katika miji ya chini ya ardhi, shambulio lolote dhidi ya vituo hivi linaweza kusababisha mlipuko mikubwa sawa na “tetemeko kubwa la ardhi.”

Kwa maneno mengine, hata shambulio moja la moja kwa moja linalolenga kambi hizi zilizo chini linaweza kusababisha uharibifu mkubwa.

Zaidi ya hayo, makombora mengi ya Jamhuri ya Kiislamu yako chini ya ardhi na hayawezi kuharibiwa kwa urahisi.

Pia ni muhimu kutambua kwamba, tofauti na vituo vya nyuklia ambavyo vilikuwa katika maeneo maalum na machache, vituo vya makombora vya Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi (IRGC) vimetawanyika karibu kote Iran, na kuviangamiza vyote itakuwa vigumu sana.

Bw. Azizi, ambaye ni mtafiti wa sera za kigeni katika eneo hilo, anasema:

“Wakati wa vita, Iran iligundua kuwa sio makombora yote yaliweza kufikia Israeli, ni makombora ya Fatah pekee, yaliyotumika katika siku za mwisho za vita, ndiyo yalikuwa na uwezo wa kufikia malengo kwa kiwango cha juu cha mafanikio.”

Hamidreza Azizi anaongeza kuwa maafisa wa jeshi la Iran huenda wamezidisha kutengeneza aina hii ya kombora katika kipindi cha baada ya vita.

Kuna ushahidi wa kuunga mkono hili. Novemba mwaka huu, CNN iliripoti China iliitumia Iran tani 2,000 za sodiamu perchlorate, kemikali inayotumika kutengeneza roketi imara zaidi.

Usiri wa Iran

Mambo haya yote huenda yanaifanya Israel kuwa na wasiwasi kwamba Iran inaweza kupanua uwezo wake wa makombora.

Pia, kuna ripoti kwamba siku ya Jumatatu, Iran ilifanya jaribio kombora, baadhi ya vyombo vya habari vilithibitisha na vingine vilikataa.

Hii inaonyesha upande wa Iran unajaribu kutuma ujumbe kwa Israel; ujumbe unaoonyesha utayari wa Tehran kujibu mashambulizi mapya kutoka upande mwingine.

Wakati huo huo, baadhi ya wataalamu wa masuala ya kijeshi wanaamini moja ya mabadiliko ambayo yametokea katika mfumo wa kufanya maamuzi wa Jamhuri ya Kiislamu ni aina ya usiri kuhusu uwezo wa kijeshi wa Iran, mbinu zake za utekelezaji, na mipango yake.

Hili linaendana na ripoti zinazokinzana na zisizoeleweka kuhusu majaribio ya makombora. Kwa maneno mengine, Iran inaboresha uwezo wake wa kijeshi kwa njia ya siri na kisiasa, na kufanya iwe vigumu kuelewa wazi nia yake ya kweli.

Baadhi ya vyombo vya habari vya Israeli vinavyoripoti, Iran inajiandaa kuanzisha mashambulizi dhidi ya Israeli. Lakini historia inaonyesha Iran haijawahi kuanzisha shambulio dhidi ya Israel.

Zaidi ya hayo, baada ya vita vya siku 12, Tehran bado haijaweza kujenga upya uwezo wake dhaifu wa ulinzi. Kwa hivyo, inaonekana haiwezekani Iran kuanzisha shambulio wakati huu.

Netanyahu anataka nini?

cx

Chanzo cha picha, Reuters

Je, Benjamin Netanyahu atajaribu kumshawishi Donald Trump kuanzisha shambulio lingine la kijeshi dhidi ya Iran wakati wa ziara yake nchini Marekani, kama baadhi ya vyombo vya habari vya Israeli na Marekani vinavyoripoti?

Katika hali ilivyo sasa: Je, mpango wa makombora wa Iran ni tishio la moja kwa moja kwa usalama wa Israel, na kumfanya rais wa Marekani kuanzisha shambulio lingine dhidi ya Iran ili kuiangamiza?

Hamidreza Azizi, akizungumzia juu ya kubadilika kwa mikakati ya Israeli baada ya tukio la Oktoba 7, anasema:

“Israeli haiuoni tena tofauti kati ya vitisho vya muda mfupi na vya muda mrefu. Inavichukulia hata vitisho vya muda mfupi kwa uzito mkubwa na inachukua hatua za kuviondoa.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *