Baada ya Marekani kuituhumu Rwanda kwa kukiuka makubaliano ya amani iliyosaini na jirani yake mapema Desemba, M23 ilisema ingejiondoa Uvira.

Lakini waasi wa M23 wakiwa wamevalia kiraia wamebaki mjini humo, kwa mujibu wa vyanzo vya eneo hilo na kiusalama.

Kiongozi wa asasi za kiraia Martin Mafikiri Mashimango amesema, takribani saa 12 asubuhi, boti mbili za doria za M23 zilishambuliwa katika bandari ya Kalundu kabla ya kushika moto.

Lakini pia chanzo kingine cha usalama cha DRC kiliiambia AFP kwa sharti la kutotajwa jina kwamba hizo zilishambuliwa na droni zao katika eneo la Kalundu bandari iliyo kwenye Ziwa Tanganyika.

Kongo na Rwanda: Nini kipo kwenye mkataba wa amani?

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Wapiganaji wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda walikuwa wameteka mji huo muhimu karibu na mpaka wa Burundi mapema mwezi huu, muda mfupi baada ya serikali za Congo na Rwanda kusaini makubaliano ya amani mjini Washington ambayo Rais wa Marekani Donald Trump aliita ‘muujiza mkubwa.

Makabiliano kati ya M23 na wapiganaji wanaoiunga mkono serikali yalizuka mapema wiki hii karibu na Uvira wakati wapiganaji wanaoungwa mkono na Rwanda na wapiganaji wanaoiunga mkono Kinshasa wakifahamika kama Wazalendo walishambuliana kwa makombora ambayo yalisikika hadi Uvira, kwa mujibu wa Mashimango.

Jeshi la DRC limeita ahadi ya kujiondoa kwa M23 kuwa ni “mapinduzi ya vyombo vya habari yaliyokusudiwa kudanganya mtizamo wa umma” na kulishutumu kundi hilo kwa kujipanga upya katika vilima vilivyo juu ya Uvira.

AFP

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *