Marekani imefanya mashambulizi ya anga dhidi ya wapiganaji wa Islamic State (ISIS) kaskazini magharibi mwa Nigeria, Rais Donald Trump ametangaza kwenye jukwaa lake la mtandao wa kijamii, Truth Social, siku ya Alhamisi, Desemba 25, akiwatuhumu kwa kuwaua Wakristo katika eneo hilo. Wanadiplomasia wa Nigeria wamethibitisha “mashambulizi sahihi ya Marekani dhidi ya malengo ya kigaidi, kama sehemu ya ushirikiano wa usalama na Marekani.”

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Na: RFI na mashirika mengine

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Alhamisi, Desemba 25, rais Trump ametangaza kwamba Marekani imefanya mashambulizi “mengi” ya anga yaliyosababisha vifo vingi katika safu ya wapiganaji wa Islamic State kaskazini magharibi mwa Nigeria na kuahidi mashambulizi zaidi ikiwa kundi hilo litaendelea kuwaua Wakristo nchini humo.

“Hapo awali niliwaonya magaidi hawa kwamba ikiwa hawatasitisha mauaji ya Wakristo, watakiona cha mtema kuni, na usiku wa leo wamepigwa san,” Donald Trump ametangaza kwenye jukwaa lake la Truth Social, akiongeza kuwa “Wizara ya Vita ilifanya mashambulizi mengi sahihi.”

“Usiku wa leo, kwa maelekezo yangu kama Amiri Jeshi Mkuu, Marekani imezindua shambulio lenye nguvu na hatari kaskazini magharibi mwa Nigeria dhidi ya wanyama waharibifu wa kigaidi wa Daesh, ambao waliwalenga na kuwaua kikatili, hasa Wakristo wasio na hatia, katika viwango ambavyo havijaonekana kwa miaka mingi, labda hata karne nyingi!” Trump ameandika kwenye mtandao wake wa social Truth.

“Kamandi ya jeshi la Marekani barani Afrika imesema kupitia mtandao wa kijamii wa X kwamba shambulio hilo limezinduliwa kwa ombi la mamlaka ya Nigeria. Wapiganaji kadhaa wa ISIS waliuawa katika Jimbo la Sokoto,” imeongeza. Video iliyotolewa na Pentagon inaonyesha angalau kombora moja likirushwa kutoka kwa meli ya kivita. Mwakilishi wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani amesema kwamba wapiganaji wengi walioko katika kambi ya ISIS walilengwa.

Mkuu wa Pentagon Pete Hegseth ametoa shukrani zake kwa msaada na ushirikiano wa serikali ya Nigeria, akisifu hatua za wizara yake. Diplomasia ya Nigeria imethibitisha mashambulizi ya usahihi ya Marekani dhidi ya malengo ya kigaidi. Wizara ya Mambo ya Nje ya Nigeria imesema kwamba mashambulizi hayo yalifanywa “kama sehemu ya ushirikiano wa usalama na Marekani,” ikibainisha kwamba ushirikiano huu unaoendelea unahusisha ushiriki wa akili na uratibu wa kimkakati ili kulenga makundi yenye silaha. “Hii imesababisha mashambulizi ya usahihi dhidi ya malengo ya kigaidi nchini Nigeria kwa mashambulizi ya anga Kaskazini Magharibi,” wizara imeandika kwenye mandao wa kijamii wa X.

Mashambulizi haya yanaashiria uingiliaji kati wa kwanza wa kijeshi wa Marekani katika nchi yenye watu wengi zaidi barani Afrika chini ya utawala wa Donald Trump. Rais wa Marekani amekuwa akionya tangu mwishoni mwa mwezi Oktoba kuhusu kile anachokielezea kama “tishio la kuwepo” kwa Ukristo nchini Nigeria. Hapo awali alisema kwamba anafikiria kuingilia kati kijeshi katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, akikosoa mamlaka za nchi hiyo kwa kutofanikiwa kwao katika kupambana na vurugu dhidi ya jamii za Wakristo.

Uingiliaji kati ulioandaliwa na Washington

Mnamo Desemba 22, shirika la habari la Reuters liliripoti kwamba Washington ilianza kufanya safari za ndege za kukusanya taarifa za kijasusi katika sehemu kubwa za eneo la Nigeria mnamo mwezi Novemba. Serikali ya Nigeria hapo awali ilisema kwamba makundi yenye silaha yanawalenga Waislamu na Wakristo, ikisema kwamba uonyeshaji wa Washington wa mateso ya Wakristo hauonyeshi ugumu wa hali ya usalama na unapuuza juhudi za kulinda uhuru wa kidini.

Hata hivyo, Abuja imekubali kufanya kazi na Marekani ili kuimarisha uwezo wake wa kupambana na makundi yenye silaha. Nigeria imegawanywa kwa usawa kati ya kusini yenye Wakristo wengi na kaskazini yenye Waislamu wengi. Ni eneo la migogoro mingi inayowaua Wakristo na Waislamu, mara nyingi bila kubagua. Kwa upande wake, Abuja inafutilia mbali madai haya ya mauaji ya Wakristo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *