Michuano ya kandanda ya mataifa barani Afrika AFCON 2025 inaendelea hii leo kwa mechi za mzunguko wa pili katika viwanja mbalimbali nchini Morocco.

Mechi ya awali kabisa hii leo ni kati ya Angola dhidi ya Zimbabwe, timu hizi za kundi zinakutana baada ya kila mmoja kuchapwa katika mechi zao za mzunguko wa kwanza. Baadaye jioni kutakuwa na mechi mbili za kundi hilo hilo kati ya vigogo Misri dhidi ya Afrika Kusini. 

Katika mechi za kundi A, mechi ya awali itakuwa kati ya Zambia Chipolopolo ambao watamenya na visiwa vya Comorro,  mechi ya usiku na ya mwisho itawakutanisha wenyeji Morocco dhidi ya Mali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *