Mtoto mwenye umri wa miaka (3) aliyekuwa akifahamika kwa jina la Samir Adam amekutwa amefariki dunia huku mwili wake ukiwa kwenye dimbwi la maji katika mtaa wa kizigo kata ya Ng’ambo Manispaa ya Tabora kufuatia mvua kubwa iliyonyesha kwa zaidi ya saa nne

Wakizungumzia mazingira ya kifo cha mtoto huyo baadhi ya mashuhuda akiwemo baba mzazi wa marehemu wamesema kabla mtoto huyo hajafikwa na umauti alikuwa akicheza na watoto wenzie nyuma ya nyumba yao

Uongozi wa serikali ya mtaa alipokua akiishi marehemu umethibitisha kutokea kwa tukio hilo

Jeshi la zima moto na uokoaji mkoa wa Tabora limefika eneo lilipotokea tukio hilo la kusikitisha na kutoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari kwenye maeneo hatarishi hasa wakati huu wa msimu wa mvua za masika zinazoendelea kunyesha.

✍️ @pendo-salu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *