Myanmar itafanya awamuya kwanza ya uchaguzi mkuu wake wa kwanza katika kipindi cha miaka mitano Jumapili hii, katika hatua ambayo wa wakosoaji wanasema halitarejesha demokrasia dhaifu ya nchi hiyo iliyoporomoka baada ya mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2021, na kadhalika haitamaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyochochewa na utawala mkali wa kijeshi. Upigaji kura utafanyika katika sehemu mbalimbali za nchi kwa awamu tatu, ambapo awamu ya pili itakuwa Januari 11 na ya tatu Januari 25.Wakosoaji wanatia shaka kuhusu uwezekano wa mabadiliko halisi kuelekea utawala wa kiraia.Makundi ya haki za binadamu na upinzani yanasema uchaguzi huo hautakuwa huru wala wa haki na kwamba mamlaka huenda ikabaki mikononi mwa kiongozi wa kijeshi Jenerali Mkuu Min Aung Hlaing.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *