
Wizara ya Mambo ya Nje ya Nigeria ilithibitisha siku ya Ijumaa kuwa mashambulizi ya angani yaliyofanya na Marekani dhidi ya magaidi yalilenga shabaha katika eneo la kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo, na ikaongeza kuwa bado inaendelea kushirikiana katika masuala ya kiusalama na Marekani.
Usiku wa kuamkia Ijumaa Rais wa Marekani amesema nchi yake ilifanya mashambulizi mengi yaliyolenga shabaha dhidi ya Daesh kaskazini-magharibi mwa Nigeria, akidai kuwa kundi hilo limekuwa likiwalenga Wakristo.
“Usiku wa leo, kwa maelekezo yangu kama Amiri Jeshi Mkuu, Marekani ilianzisha shambulizi kali dhidi ya magaidi wa ISIS (Daesh) kaskazini-magharibi mwa Nigeria, ambao wamekuwa wakilwalenga na kuwaua kikatili, hasa Wakristo wasio na hatia,” Trump alisema kupitia mtandao wa kijamii wa Truth Social siku ya Alhamisi.
“Nilikuwa nimewaonya magaidi hawa hapo awali kwamba kama hawataacha mauaji ya Wakristo, kutakuwa na adhabu kali, na usiku wa leo, adhabu hiyo imetolewa.”
Aliongeza kuwa “hilo ni jambo ambalo ni Marekani pekee inayoweza kulifanya.”
Hata hivyo mamlaka za Nigeria na watafiti wamekuwa wakipinga mara kwa mara madai ya Trump kwamba magaidi wanawalenga Wakristo hasa nchini Nigeria, wakisema kuwa makundi ya kigaidi hufanya mashambulizi bila kubagua raia, bila kujali dini zao.
Kuonyesha ubabe wa Marekani