s

Chanzo cha picha, Sky

Muda wa kusoma: Dakika 2

Manchester City wanaongozwa mbio za kumsaini Antoine Semenyo, huku Benfica, Manchester United na Liverpool bado wanavutia mshambuliaji huyo wa Bournemouth. (GIVEMESPORT)

Manchester United sasa wanaangalia uwezekano wa kumnasa winga Yan Diomande wa RB Leipzig kama mbadala wa Semenyo baada ya ripoti kuonyesha City ndio waliopo mbele katika mbio za kumsaini staa huyo wa Bournemouth. (GIVEMESPORT)

Chelsea na yenyewe imefanya uchunguzi wa awali juu ya Semenyo wakati timu kama Tottenham tayari ikijiondoa kwenye harakati za kumsajili. (GIVEMESPORT)

Mohamed Salah anaendelea kuvutia klabu za Uarabuni wakati yuko Morocco kwa ajili ya mashindano ya AFCON, huku timu mbili za Mashariki ya Kati zikionyesha nia ya kumsaini. (Goal)

s

Chanzo cha picha, Goal

Arsenal wameongeza msukumo wa kumsajili kipa Diant Ramaj, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo Heidenheim, huku wasaka vipaji wa the Gunners wakiripotiwa kutembelea Ujerumani mara kadhaa hivi karibuni. (goal.com)

Kocha wa Manchester United Ruben Amorim anaamini Kobbie Mainoo bado ana nafasi kwenye klabu hiyo, akionyesha hana mpango wa kumuuza Januari licha ya uvumi kwamba anataka kuondoka. (Sky Sports)

AS Roma wanaandaa pendekezo rasmi kumchukua Joshua Zirkzee kwa mkopo, kwa sharti la kumnunua moja kwa moja baadaye. (Sky Italia)

Bayern Munich wanavutiwa na kinda wa Cardiff City Dylan Lawlor, ambaye anatajwa kwa kasi yake kwenye nafasi ya ulinzi, huku klabu hiyo ya Ujerumani ikiendelea kufuatilia maendeleo yake. (talkSPORT)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *