RSF ilianza mashambulizi yake mapema siku ya Alhamisi katika eneo hilo, lakini vikosi vilivyokuwa vinalinda vilifanikiwa kutibuwa mashambulizi hayo tena, na kuwakabili vikali wapiganaji hao, magari yao na vifaa kuwalazimisha kurudi nyuma, vikosi hivyo washirika vilisema.

Mashambulizi hayo yanakuja huku RSF ikitaka kuchukuwa udhibiti kamili wa Darfur Kaskazini. Jeshi la Sudan na vikosi washirika linadhibiti maeneo matatu kwenye jimbo hilo — Ambro, Karnoi na Tina — huku Sudan Liberation Movement inayoongozwa na Abdel Wahid al-Nur likidhibiti eneo la Tawila.

Mapigano yalitokana na RSF kuchukuwa udhibiti wa El-Fasher Oktoba 26, ambapo mashirika ya maeneo hayo na kimataifa yameripoti mauaji ya kikatili kwa raia, kusababisha onyo kutolewa kuhusu hatari ya mgawanyiko zaidi nchini Sudan.

Majimbo matatu ya Kordofan—Kaskazini, Magharibi, na Kusini —yamepitia wiki kadhaa za mapigano makali kati ya jeshi na RSF, kulazimisha maelfu ya watu kukimbia maeneo hayo.

Mapigano kati ya jeshi la Sudan na RSF, ambayo yalianza Aprili 2023, yamesababisha vifo vya maelfu ya watu na mamilioni wengine kuondoka katika makazi yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *