Viongozi wa Dini watakiwa kupinga chukiViongozi wa Dini watakiwa kupinga chuki

WAZIRI Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba ametoa wito kwa viongozi wa dini kuendelea kushirikiana na serikali katika kutoa elimu ya umoja na amani, kupinga chuki, migawanyiko na vitendo vyovyote vinavyoweza kuvuruga mshikamano wa taifa.

Amesema kuwa vita yoyote inayohusisha wenyewe kwa wenyewe huwa haina mshindi bali ina kupoteza wote na mgawanyiko ndani ya taifa hauna mshindi bali una matokeo ya kushindwa wote kama taifa. SOMA Askofu Mlola:Tusiharibu tunu ya amani

: Ametoa wito huo jana aliposhiriki ibada ya Krismasi katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Kanisa Kuu la Azania Front Dar es Salaam. “Manufaa ya amani ni makubwa, huleta maendeleo ya kiuchumi, huimarisha ustawi wa jamii na huwezesha kila Mtanzania kushiriki kikamilifu katika kujenga taifa,” alisema.

Alisema serikali inaendelea kutekeleza wajibu wake wa kulinda amani na usalama wa nchi pamoja na kuwajenga Watanzania hususani vijana kuthamini dhana ya uzalendo kwa nchi. “Tanzania imeendelea kuwa kielelezo cha umoja, amani, mshikamano na utulivu katika ukanda wetu na Afrika. Amani hii imejengwa juu ya misingi imara ya maadili, haki, kuheshimiana, uvumilivu na uzalendo,” alisema.

Kadhalika, Dk Mwigulu ametoa wito kwa wazazi na walezi kuendelea kushirikiana kwa karibu na taasisi za elimu na dini katika kuimarisha malezi ya watoto na vijana kwa kuwajengea misingi imara ya maadili na kuwaongoza kutumia vyema fursa za elimu, teknolojia na utandawazi kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *