WAKATI waumini wa dini ya Kikristo nchini na duniani wakiendelea kusherehekea Sikukuu ya Krismasi ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, watoto 13 wamezaliwa nchini katika hospitali mbalimbali.

HabariLEO ilizungumza na maofisa habari kutoka katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Mwananyamala, Agakhan na Hospitali ya Palestina kujua idadi ya watoto waliozaliwa katika usiku huo sambamba na siku ya kuzaliwa kwa Kristo.

Akizungumza na HabariLEO jana, Ofisa Habari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala, Florian Godwin alisema katika hospitali hiyo usiku wa kuamkia Desemba 25, walizaliwa watoto watatu, wawili wakiwa ni wa kike na mmoja wa kiume. SOMA: Walindeni watoto ufukweni

Pia, Onesmo Milanzi kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke amesema katika hospitali hiyo alizaliwa mtoto mmoja wa kike mwenye uzito wa kilo 2.8 na alizaliwa kwa njia ya upasuaji. “Mama pamoja na mtoto wake wanaendelea vizuri chini ya uangalizi wa madaktari na wauguzi wa hospitali yetu,” alisema Milanzi.

Kwa upande wake Olayce Lotha wa Hospitali ya Rufaa ya Agakhan alisema usiku huo katika hospitali hiyo walizaliwa watoto watano wa kike wakiwa wanne na mmoja wa kiume. Pia, katika Hospitali ya Palestina ilielezwa kuwa watoto waliozaliwa kwenye usiku wa kuamkia sikukuu hiyo walikuwa ni wanne.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *