Morocco ambayo ilihitaji ushindi ili kujihakikishia tiketi ya moja kwa moja ya hatua ya 16 bora, ilijikuta ikipata presha kubwa kutoka kwa Mali ambayo ilicheza kwa nidhamu na kasi kipindi chote cha mchezo.

Hadi sasa, Morocco bado haijathibitisha nafasi yake katika hatua ya mtoano, ingawa inaongoza Kundi A ikiwa na pointi nne baada ya kucheza mechi mbili. Mali inafuata ikiwa na pointi mbili, sawa na Zambia, ambayo ilitoka sare ya 0–0 dhidi ya Comoro mjini Casablanca.

Morocco itamenyana na Zambia Jumatatu, na ushindi dhidi ya mabingwa hao wa mwaka 2012 utaihakikishia timu hiyo ya wenyeji kufuzu kama vinara wa kundi.

Leo hii ni zamu ya Benin kukipiga na Botwana, kisha Senegal ikutane na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mechi nyengine itawakutanisha majirani wa Afrika Mashariki Uganda na Tanzania na kisha baadaye Nigeria itaingia uwanjani kuvaana na Tunisia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *