Mvutano umeendelea kutanda na kuwa mkubwa siku ya Ijumaa, Desemba 26, huko Uvira, katika mkoa wa Kivu Kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Wakati wapiganaji wa AFC/M23 walipaswa kuondoka jijini Uvira mnamo Desemba 16, milio ya risasi ilisikika tena hadi adhuhuri. Tofauti na siku mbili zilizopita, ambazo shughuli zilirudi kwa kasi, wakazi walibaki ndani. Shughuli nyingi zikisitishwa kwa siku nzima ya jana.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Matukio ya kwanza yaliripotiwa yapata saa 12:00 asubuhi. Boti mbili za mwendo kasi zilizotia nanga katika bandari ya Kalundu, bandari kuu ya Uvira, zilipigwa na makombora na kushika moto.

Kulingana na AFC/M23, ambayo inadai kuwa haina kikosi cha majini, meli zilizohusika zilikuwa za raia. Kundi hulo la waasi linaishutumu Kinshasa kwa kuwalenga raia. Kwa upande wao, vyanzo vya FARDC vilivyowasiliana na RFI vinaonyesha kuwa mashambulizi hayo yalifanywa kwa kutumia ndege zisizo na rubani na kudai kuhusika na mashambulizi hayo.

Kulingana na jeshi la Kongo, meli hizi zilikuwa zikitayarishwa kushambulia vitengo vya jeshi la FARDC vilivyokuwa karibu na Katongo, takriban kilomita kumi kutoka Uvira, ambapo mapigano pia yaliripotiwa na vyanzo huru.

Vikosi vya AFC/M23 vyaripoti ndani na nje ya jiji la Uvira

Mchana, ndege iliyokuwa ikiruka juu ya anga ya Uvira ilizua hofu miongoni mwa wakazi. Vyanzo vya ndani vinadai bado vinawaona watu wakiwa wamevaa sare za polisi za AFC/M23, ingawa vifaa vizito vya kundi hilo na sehemu kubwa ya vikosi vyake vimeripotiwa kuondoka jijini. Walipoulizwa kuhusu uwepo huu wa wanajeshi wa M23 waliobaki, kundi hilo lenye silaha halikujibu.

AFC/M23 pia inawashutumu wapiganaji wa Wazalendo, wanaoshirikiana na vikosi vya serikali, kwa kujiweka katika vilima vinavyozunguka Uvira na kupanga mashambulizi kutoka katika vilima hivyo.

Kulingana na vyanzo vya kijeshi, uwepo mkubwa wa AFC/M23 pia umeripotiwa huko Kiliba. FARDC (Vikosi vya Jeshi vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) wanasema kwamba wataingia mjini humo katika siku zijazo, “kitaalamu na bila haraka.”

Kusini zaidi, katika mji wa Makobola, pande zote mbili za Fizi na Uvira, maeneo hayo yamekuwa chini ya udhibiti wa FARDC (Vikosi vya Jeshi vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) na Wazalendo tangu Alhamisi, Desemba 25, saa 9:00 alaasiri.

Krismasi chini ya mvutano mkali

Hali bado haitabiriki. Kwa mfano, hakuna Misa ya Krismasi iliyosherehekewa. Maagizo yalitolewa kwa ibada za kidini kufanyika kati ya saa 10:00 na saa 7:00 jioni pekee. Parokia za Sange, kaskazini, na Makobola, kusini, hazikufanya ibada.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *