Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amewapongeza viongozi wote katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ambao wanajitolea kwa hali na mali kuisaidia Jamii kwa matendo na kuigusa Moja kwa moja kama inavyoelekeza ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM)
Mpogolo ametoa pongezi hizo akiwa kata ya Zingiziwa Jimbo la Ukonga Jijini Dar es salaam wakati wa Zoezi la Kukabidhiwa nyumba ya Kisasa ya Kuishi Mjane Fatuma Msham ,Nyumba aliyojengewa na Diwani wa Kata ya Zingiziwa Selemani Kaniki ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa kwa mama huyo ambaye hapo kabla alikuwa ikiishi kwenye nyumba ya Matope.
Dc Mpogolo alisema Rais wa Tanzania ameelekeza kujali na kutatua shida za watanzania hivyo amewataka viongozi wasichoke kuhudumia watu bali washirikiane kwa kutafuta namna bora ya Kuzitatua changamoto na Kuboresha Maisha ya Watanzania.
Kwa Upande wake Diwani kata ya Zingiziwa Seleman Kaniki (CCM) alisema ataendelea Kushirikiana na wananchi kwa nguvu zote ili kuunga mkono Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia suluhu Hasani.
Ikumbukwe pia Chama cha Mapinduzi (CCM) Katika Ilani yake ya 2025–2030, kimepanga kuanzisha programu maalum ya ujenzi wa nyumba kwa ajili ya watumishi wa sekta za kitaalamu na vyombo vya ulinzi na usalama, wakiwemo walimu, madaktari, polisi, wauguzi na watumishi wa mahakama.
Kwa mujibu wa Ilani hiyo, kutaanzishwa miradi ya nyumba za gharama nafuu, lengo ni kuwawezesha kumiliki makazi bora kabla ya kustaafu.
#kilichoborakabisa