Utawala wa Palestina umepinga vikali na kulaani kutambuliwa kwa Somaliland na taifa haramu la ukandamizaji la Israel.
Kupitia taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya nje kwenye mtandao wa X, Palestina imesema pia inapinga hatua zozote zinazounga mkono utengano au kudhalilisha uhalali wa Somalia , au zinazodhoofisha mamlaka na umoja wa Somalia na kuyumbisha usalama wake.
‘‘Wizara ya Mambo ya Nje ya Taifa la Palestina inathibitisha uungaji mkono wake kamili kwa umoja, mamlaka na uhuru wa kisiasa wa Somalia, na kuhakikisha haki ya watu wa Somalia ya maisha yenye heshima, usalama na utulivu, kulingana na sheria za kimataifa,’’ilisema taarifa hiyo.
Wizara hiyo ilisema kuwa utambuzi huo uliokataliwa unathibitisha majaribio ya Israel, kama nguvu ya kikoloni inayofanya kazi ya kudhoofisha amani na usalama wa kimataifa, haswa usalama wa kikanda na wa Kiarabu.