
Onyo hilo limetolewa kufuatia mashambulizi ya anga yanayodaiwa kufanywa na Saudi Arabia katika eneo la Hadramawt, huku Marekani ikitoa wito wa kujizuia na kuendeleza diplomasia.
Vikosi vya wanaotaka kujitenga vinavyoungwa mkono na Umoja wa Falme za Kiarabu vimepiga hatua kubwa katika wiki za hivi karibuni, jambo ambalo wachambuzi wanasema limeiweka Saudi Arabia katika hali ya kudhalilika.
Mafanikio ya vikosi hivyo yameongeza mvutano kati ya Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu, ambazo zinaunga mkono makundi tofauti ndani ya serikali ya Yemen, huku wote wakipinga waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran.