Shirika la Kutetea Haki za Binadamu nchini Ethiopia, la Human Rights First limeishtaki serikali ya Ethiopiia kwa kile lilichodai hatua ya serikali ya Addis Ababa ya kuwatelekeza wakimbizi.

 Human Rights First, limefungua kesi dhidi ya Baraza la Mawaziri la serikali ya Muungano, Wizara ya Amani, na serikali za kikanda za Tigray, Amhara, na Oromia.

Shirika hilo linazishutumu mamlaka hizo kwa kushindwa kuwarejesha wakimbizi wa ndani zaidi ya milioni 1.5 walio chini ya utawala wao kwenye makazi yao.

Katika kesi yake iliyowasilishwa katika Mahakama Kuu ya Ethiopia, shirika hilo linaonyesha kuwa katika eneo la Tigray pekee, zaidi ya wakimbizi milioni moja wa ndani wamesalia bila makazi kutoka eneo la Tigray magharibi kufuatia kuzuka kwa vita vya Tigray mnamo Novemba 4, 2020.

Shirika hilo limebainisha zaidi kwa kusema kwamba katika eneo la Amhara, zaidi ya wakimbizi nusu milioni waliokimbia kutoka eneo la Oromia katika mji wa Debre kwa sasa wanaishi katika mji wa Berhan.

Huko Oromia kwenyewe, takriban wakimbizi 85,000 kutoka sehemu mbalimbali za nchi wanaishi katika makazi ya muda.

Human Rights First pia inazishutumu mamlaka za kitaifa na kikanda kwa kupuuza wajibu wao wa kuwawezesha wakimbizi hao kurudi salama makwao, baada ya  kuwaacha wakiteseka kutokana na matatizo mengi ya kijamii wanayokabiliiwa nayo.

Kulingana na shirika hilo, makazi hayo ya muda hayana maji ya kutosha, chakula, vyoo, elimu na vituo vya afya, hali ambayo inahatarisha maisha ya wakimbizi hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *