Makubaliano hayo yanazitaka pande zote kusitisha harakati za kijeshi na kutoingia anga ya upande mwingine. Pia yanaitaka Thailand baada ya saa 72 za utulivu, kuwarejesha wanajeshi 18 wa Cambodia waliokamatwa mwezi Julai—jambo ambalo limekuwa likitiliwa mkazo na Cambodia.

Makubaliano hayo yalisainiwa na mawaziri wa ulinzi wa nchi hizo baada ya mazungumzo ya siku tatu ya maafisa wa kijeshi. Viongozi hao pia wamethibitisha kujitolea kwao kuheshimu usitishaji wa mapigano wa awali na kutekeleza hatua 16 za kupunguza mvutano.

Aidha makubaliano hayo mapya yanazitaka pande zote kuheshimu mikataba ya kupiga marufuku mabomu ya ardhini, kuepuka kusambaza habari za uongo, kuendelea na mipango ya kuweka mipaka, na kushirikiana kupambana na uhalifu wa kimataifa—hasa ulaghai wa mtandaoni unaoendeshwa na magenge ya uhalifu nchini Cambodia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *