Thailand na Cambodia zimekubaliana leo Jumamosi, Desemba 27, “kusitisha mapigano mara moja” katika mzozo wao wa mpaka, kulingana na taarifa iliyosainiwa na miji mikuu hii miwili na kupatikana na shirika la habari la AFP kupitia Cambodia. Mapigano hayo yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 47 na karibu milioni moja kuhama makazi yao katika kipindi cha wiki tatu.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wakilazimishwa kulala kwenye mahema au katika makazi ya dharura yaliyojaa watu tangu mapigano yalipoanza tena Desemba 7, mamia ya maelfu ya watu waliohamishwa pande zote mbili za mpaka unaozozaniwa wanaweza kutumia Mwaka Mpya nyumbani.

“Pande zote mbili zinakubaliana kusitisha mapigano mara moja baada ya kusainiwa kwa tamko hili la pamoja, linaloanza kutumika saa 6:00 mchana (saa za ndani, au 12:00 asubuhi saa za Ufaransa) mnamo Desemba 27, 2025,” inasema hati hiyo, iliyosainiwa na mawaziri wa ulinzi wa majirani hao wawili wa Kusini Mashariki mwa Asia. “Pande zote mbili zinakubaliana kuwaruhusu raia wanaoishi katika maeneo ya mpaka yaliyoathiriwa kurudi nyumbani haraka iwezekanavyo, bila kizuizi, na kwa usalama na heshima,” tamko la pamoja linaongeza.

Nakala hiyo pia inataja kuzuiwa kwa ngome za kijeshi, kuondolewa kwa mabomu kutoka maeneo ya mpaka, na ushirikiano wa polisi ili kupambana na uhalifu wa mtandaoni. Pande zote mbili zinaahidi kukomesha mashambulizi yote na kuzuiwa kwa nngome za wanajeshi, bila harakati yoyote au uimarishaji. Ikiwa kusitisha mapigano, kwa sasa ni kwa muda, kutadumu kwa saa 72, Thailand imeahidi kuwaachilia huru wanajeshi 18 wa Cambodia waliokamatwa tangu kuzuka kwa ghasia kwa mara ya kwanza mwezi Julai mwaka huu, anaripoti mwandishi wetu huko Bangkok, Valentin Cebron.

Amani dhaifu

Kulingana na takwimu rasmi za hivi karibuni, jumla ya watu 47 wliuawa katika wiki tatu zilizopita: 26 upande wa Thai na 21 upande wa Cambodia. Mapigano ya kwanza mwezi Julai yalsababisha vifo vya watu 43 katika siku tano kabla ya makubaliano ya kusitisha mapigano kufikiwa, hasa kutokana na kuingilia kati kwa Donald Trump. Makubaliano ya kusitisha mapigano yalitiwa saini Oktoba 26 huko Kuala Lumpur, mbele ya rais wa Marekani, lakini yalisitishwa wiki chache baadaye na Thailand baada ya wanajeshi wake kadhaa kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu la ardhini kwenye mpaka.

Pia zikiwa zimeshinikizwa na China kukomesha mzozo huo, Thailand na Cambodia hatimaye zilikubaliana kufanya mazungumzo ya moja kwa moja baada ya mkutano wa dharura wa mawaziri wa mambo ya nje wa ASEAN siku ya Jumatatu.

Hata hivyo, suala la uwekaji mipaka na uhuru wa mahekalu kadhaa ya kale, ikiwa ni pamoja na Preah Vihear iliyoorodheshwa na UNESCO, bado halijatatuliwa na linaibua mashaka kuhusu uwezekano wa muda mrefu wa kusitisha mapigano. Nchi hizo mbili zina mgogoro wa muda mrefu kuhusu mpaka wao wa kilomita 800, ulioanzishwa wakati wa kipindi cha ukoloni wa Ufaransa, na zinashutumiwa kila mmoja kwa kusababisha ongezeko hili la hivi karibuni la vifo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *