Mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, umelengwa na shambulio la ndege isiyo na rubani ya Urusi na kombora lililomuua mtu mmoja usiku wa Ijumaa, Desemba 26 kuamkia Jumamosi, Desemba 27. Wimbi la mashambulizi lilitokea siku moja kabla ya mkutano uliopangwa kufanyika siku ya Jumapili huko Florida kati ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Rais wa Marekani Donald Trump kujadili suala nyeti la maeneo yanayokaliwa na Urusi, ndani ya mfumo wa mazungumzo yanayolenga kukomesha vita.

Imechapishwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Karibu miaka minne baada ya uzinduzi wa shambulio kubwa la Urusi, Ukraine inakabiliwa na mashambulizi ya mabomu kila siku. Kwa zaidi ya makombora 40 ya hypersonic, ballistiska, na cruise na zaidi ya ndege 500 zisizo na rubani,  Kyiv kwa mara nyingine tena inalengwa na Urusi. Kufikia saa sita mchana, idadi ya vifo ilikuwa imeongezeka hadi angalau 28, na watu wamekwama chini ya vifusi huku timu za uokoaji zikiendelea kuwepo katika eneo la tukio, anaripoti mwandishi wetu huko Kharkiv, Emmanuelle Chaze. Majengo ya makazi yalipigwa moja kwa moja na ndege zisizo na rubani, na moto ulizuka katika vitongoji kadhaa vya jiji. Miundombinu ya nishati ya Kyiv, ambayo tayari ilikuwa imeathiriwa na mashambulizi ya awali, ilizidiwa, na sehemu za jiji hazikuwa na umeme na joto.

Vitali Klitschko, meya wa mji mkuu, ambapo moto ulianza katika jengo la makazi, ameongeza kuwa “majengo ya ghorofa 2,600, vituo 187 vya kulelea watoto, shule 138, na vituo 22 vya huduma za kijamii” havikuwa na joto. Shambulio hilo pia limegharimu maisha ya mwanamke mwenye umri wa miaka 47 katika jimbo la Kyiv, kulingana na gavana wajimbo hilo, Mykola Kalashnyk, ambaye ameongeza kuwa “zaidi ya kaya 320,000 hazina umeme.”

Jeshi la Anga la Ukraine lilitoa tahadhari ya anga ya nchini humo mapema Jumamosi na kusema kwenye mitandao ya kijamii kwamba ndege zisizo na rubani na makombora zilikuwa zikirushwa juu ya maeneo kadhaa ya Ukraine, ikiwa ni pamoja na mji mkuu.

Urusi “haitaki kukomesha vita”

Shambulio la ndege zisizo na rubani na makombora la Urusi lililolenga Kyiv linaonyesha kuwa Urusi “haitaki kukomesha vita,” ameongeza Volodymyr Zelensky. Anadai kwamba Urusi “inatafuta kila fursa ya kuisababishia mateso zaidi Ukraine.”

Rais wa Ukraine alizungumza kabla ya kuondoka kwake kwenda Marekani, ambapo amepangwa kukutana na Donald Trump kujadili mpango wa kukomesha mzozo wa Urusi na Ukraine. Mazungumzo yanayolenga kutatua mzozo huo yameongezeka katika wiki za hivi karibuni, kufuatia uwasilishaji wa mpango uliofichuliwa na Donald Trump. Ingawa hati hii hapo awali ilizingatiwa na Kyiv na nchi za Ulaya kuwa na upendeleo mkubwa kwa Moscow, Volodymyr Zelensky wiki hii alifichua maelezo ya toleo lililorekebishwa, ambalo limekosolewa na Moscow, ambayo iliishutumu Ukraine kwa kujaribu “kuharibu” mazungumzo. Toleo hili jipya linataka kusitishwa kwa mstari wa mbele bila kutoa suluhisho la haraka kwa madai ya maeneo ya Urusi, kwani Urusi inachukua zaidi ya 19% ya Ukraine.

“Tuna ratiba yenye shughuli nyingi. Itafanyika mwishoi mwa wiki hii, siku ya Jumapili nadhani, huko Florida, ambapo tutakuwa na mkutano na Rais Trump,” mkuu wa nchi wa Ukraine aliwaambia waandishi wa habari siku ya Ijumaa. Ofisi yake baadaye ilithibitisha kwamba mkutano huo “ulipangwa” kufanyika Jumapili huko Florida, ambapo rais wa Marekani anatumia likizo katika hoteli yake ya Mar-a-Lago.

“Masuala nyeti” kuhusu hatima ya Donbas

Kulingana na Volodymyr Zelensky, majadiliano yatazingatia “masuala nyeti” kuhusu hatima ya Donbas, eneo la viwanda na madini mashariki mwa Ukraine linalodaiwa na Moscow, na kiwanda cha nguvu za nyuklia cha Zaporizhzhia (kusini), kinachokaliwa na wanajeshi wa Urusi.

Waawili hao pia watajadili dhamana za usalama ambazo nchi za Magharibi zinaweza kutoa kwa Ukraine kama sehemu ya makubaliano ya amani na Urusi, aliongeza. “Kuna baadhi ya masuala ambayo tunaweza kujadili tu katika ngazi ya uongozi,” rais wa Ukraine ameelezea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *