
Uganda ilipata nafasi ya kuibuka na ushindi dakika za mwisho, lakini Allan Okello alipoteza penalti muhimu.
Tanzania ilitangulia kupata bao kupitia penalti ya Simon Msuva dakika ya 59, kabla ya Uche Ikpeazu kusawazisha kwa kichwa dakika 10 kabla ya mechi kumalizika. Sare hiyo inaiacha Uganda katika hali ngumu kwenye Kundi C, huku Tanzania ikisalia kutafuta ushindi wake wa kwanza katika michuano ya AFCON.
Nigeria inaongoza kundi C baada ya kuilaza Tunisia 3-2, Senegal ipo kileleni mwa kundi D pointi sawa na DRC baada ya kutoka sare ya 1-1.
Katika mechi nyengine za makundi Gabon itakuatana na Msumbiji, Guinea ya Ikweta itakipiga na Sudan. Algeria ikutane na Burkina Faso kisha Ivory Coast ipambane na Cameroon.