Baada ya kumalizika kwa mchezo wa jana wa AFCON kati ya Tanzania na Uganda, nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, alipotoa kauli kwa waandishi wa habari alisema haoni kama atakuwa sehemu kubwa ya kikosi katika michuano ijayo ya AFCON. Kauli hiyo imeashiria wazi kuwa mashindano haya yanaweza kuwa ya mwisho kwake kuichezea timu ya taifa, akisisitiza kuwa sasa ni wakati wa kuwapa nafasi wachezaji vijana kulibeba taifa la Tanzania.