Guinea Conakry leo Jumapili inatarajiwa kufanya uchaguzi wake wa kwanza wa urais tangu baada ya mapinduzi ya kijeshi mwaka 2021. Zoezi hili linayoashiria hatua muhimu katika kipindi cha uongozi wa mpito wa nchi hiyo kuelekea katika utawala wa kikatiba.
Wananchi wa Guinea Conakry wasiopungua milioni 6.7 wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi wa leo.
Uchaguzi wa urais wa leo nchini Guinea Conakry unafanyika kufuatia kura ya maoni ya katiba ya mwezi Septemba mwaka huu ambayo imeandaa mazingira ya kurejea utawala wa kiraia, na wakati huo huo kushiriki katika kinyang’anyiro Rais wa Serikali Mpito, Jenerali Mamadi Doumbouya, mwenye umri wa miaka 41.
Doumbouya ambaye ni Kamanda wa Vikosi Malaumu mwenye uzoefu wa majukumu nje ya nchi, aliongoza mapinduzi yasiyo ya umwagaji damu Septemba 5 mwaka 2021 na kumpindua Rais wa wakati huo, Alpha Conde.
Jenerali Doumbouya anatarajiwa pakubwa kuibuka mshindi katika uchaguzi wa urais Jumapili hii.

Conde, mweye miaka 87 aliiongoza Guinea Conakry kwa muhula wa tatu mwaka 2020 kufuatia mabadiliko ya katiba yaliyokuwa na utata, hatua iliyolalamikiwa na kupingwa vikali na wananchi.
Jumla ya wagombea tisa wanashirki katika uchaguzi wa rais wa leo nchini Guinea Conakry.