#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limemzuia kuendelea na safari dereva wa lori la mizigo, Uwimpue Bonheur (33), raia wa Kigali nchini Rwanda, baada ya kukamatwa akiendesha akiwa katika hali ya ulevi mkubwa unaotajwa kuwa hatari kwa usalama wa barabara.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama, tukio hilo lilitokea Desemba 27, 2025 majira ya asubuhi katika eneo la Kihonda Kwachambo, Manispaa ya Morogoro, kwenye barabara kuu ya Morogoro–Dodoma.
Amesema wakati wa ukaguzi, vipimo vya ulevi vilionesha dereva huyo alikuwa na kiwango cha 171.7mg/100ml, kiwango kinachozidi masharti ya kisheria, hivyo polisi walilazimika kumtoa barabarani kwa usalama wake na wa watumiaji wengine wa barabara.
Uwimpue alikuwa akiendesha lori la mizigo aina ya HOWO lenye namba za usajili RAI 878 G, akitokea Kigali kuelekea Dar es Salaam.
Kamanda Mkama amesema hatua za kisheria zinaendelea, huku akitoa wito kwa madereva kuepuka kuendesha wakiwa wamelewa kwani kitendo hicho kinasababisha ajali zinazoleta vifo, majeruhi na uharibifu wa mali na miundombinu.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania