#HABARI: Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amewatia moyo wachezaji wa Taifa Stars kuendelea kupambana katika Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) inayoendelea jijini Rabat, Morocco, akisisitiza kuwa timu hiyo ina uwezo wa kupata ushindi katika mechi inayofuata dhidi ya Tunisia Disemba 30.

Makonda amenukuliwa akisema hayo baada ya Taifa Stars kumaliza mechi yao dhidi ya Uganda kwa sare ya mabao 1-1, akieleza kufurahishwa na kiwango cha mchezo kilichoonyeshwa na wachezaji pamoja na ari na nidhamu waliyonayo uwanjani.

β€œTumeona mmejituma na hakuna kukata tamaa. Mechi inayokuja dhidi ya Tunisia tutashinda,” amesema Makonda.

Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kuipa sapoti Taifa Stars ili kuhakikisha inaendelea kufanya vizuri katika mashindano hayo, huku akiwataka wachezaji kujiamini, kusahihisha makosa madogo na kupambana kwa nguvu zote ili kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika michuano hiyo ya bara la Afrika.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *