Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani shambulio la kigaidi dhidi ya waumini katika Msikiti wa Imam Ali ibn Abi Talib (AS) katika kitongoji cha Wadi al Dhahab katika mkoa wa Homs , Syria na kuuwa shahidi  watu 5 na kujeruhi wengine 21.

Esmail Baghaei, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amekumbusha msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kulaani vikali aina zote za ugaidi na itikadi kali, na kusisitiza uwajibikaji wa pande zote ambazo zimetoa jukwaa la mwendelezo, ukuaji, na kuenea kwa ugaidi na itikadi kali kupitia uingiliaji kati mbalimbali haramu, ikiwa ni pamoja na mashambulizi dhidi ya uhuru na umoja wa ardhi wa Syria na uvamizi wa baadhi ya maeneo ya nchi hiyo. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia “ametaka kutambuliwa na kuchukuliwa hatua wahusika na watoa amri ya shambulio hilo baya la kigaidi, na kubainisha uwajibikaji wa serikali ya mpito ya Syria katika suala hili.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *