Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Qatar wamezungumza kwa njia ya simu na kubadilishana mawazo kuhusu matukio ya kikanda hususan matukio ya karibuni huko Yemene. Wamesema kuwa ipo haja ya kulindwa mamlaka ya kujitawal ya ardhi nzima ya nchi hiyo.

Sayyid Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amezungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdulrhman Al Thani na wamebadilishana mawazo kuhusu masuala muhimu na nyeti ya kanda hii.

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Qatar wameeleza wasiwasi wao kuhusu hali ya Palestina na Lebabon kufuatia ukiukaji wa usitishaji vita unaofanywa na utawala wa Israel na kuendelea mashambulizi ya utawala huo dhidi ya raia wa Gaza na Lebanon.

Sayyid Abbas Araqchi na Sheikh Mohammed bin Abdulrhman Al Thani wamesisitiza kuwa kuna ulazima kwa jamii ya kimataifa kuishinikiza Israel ili iheshimu kikamilifu majukumu yake na kukomesha sera zake za mauaji ya kimbari, uvamizi na kujitanua huko Palestina.  

Araqchi na Al Thani pia wamechunguzia matukio ya karibuni huko Yemen na kueleza umuhimu wa kulindwa mamlaka ya kujitawala na umoja wa Yemen.

Hivi karibuni, vikosi vya Baraza la Mpito la Kusini (STC) vinavyoungwa mkono na Umoja wa Falme za Kiarabu vimefanikiwa kudhibiti sehemu kubwa ya majimbo ya kusini mwa Yemen baada ya makabiliano mazito na wanamgambo wanaoungwa mkono na Saudi Arabia.

Wakosoaji wanasema kwamba nchi zote mbili zinashirikiana kuigawanya Yemen kupitia mamluki wao wanaopigana katika ardhi ya nchi hiyo. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *