Mohamed Timbulo, mhitimu wa ualimu kutoka Kilinjiko Islamic College, alirejea nyumbani akiwa na matumaini ya kupata ajira.

Baada ya changamoto, mwaka 2019 aliamua kujiajiri na kuanzisha biashara ya nguo za mitumba kwenye soko la Sido, Mbeya, akianza na mtaji wa shilingi 300,000 kutoka kwa familia.

Ingawa mwanzo ulikuwa mgumu, juhudi zake zimezaa matunda, na Novemba 26 alikutana uso kwa uso na Waziri wa Maendeleo ya Vijana, akiwa miongoni mwa wajasiliamali waliopatiwa mitaji ya kuiendeleza biashara.

Mwandishi Wetu Kakuru Msimu anatuletea taarifa zaidi.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *