Mvua kubwa zilizonyesha katika maeneo mbalimbali nchini zimeathiri usafiri wa treni, zikisababisha abiria kukwama kwa muda.
Hali hiyo imeathiri madaraja ya reli ya zamani, hususan Kidete, Kilosa mkoani Morogoro, na Gulwe, Mpwapwa mkoani Dodoma.
Aidha, hitilafu ya umeme wa TANESCO na kwenye Treni za Kisasa (SGR) ilisababisha ucheleweshaji.
TRC, kupitia Mkuu wa Kitengo cha Habari, Freddy Mwanjala, amesema shirika linaendelea na ukarabati na tathmini ili kuhakikisha safari za treni zinaanza kurejea kwenye hali ya kawaida kwa usalama.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates