Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali ncini zimeleta adha kwa wananchi wa Kata ya Mapambano na Kijiji cha Masagala, Manispaa ya Tabora baada ya maji kuzidi kingo za Bwawa la Italia na kupasuka, hali iliyosababisha kuharibika kwa barabara zinazounganisha wakazi wa Ikindwa, vijiji vya Masagala, na makao makuu ya kata.
Kwa sasa, mawasiliano ya barabara yamekatika, na wananchi wanakosa njia za uhakika za kusafirisha mizigo na kupata huduma muhimu.
✍ Juma Kapipi
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates