
Rais wa Vladimir Putin wa Russia amesema kuwa Moscow iko tayari kutumia nguvu za kijeshi kufikia malengo ya operesheni yake maalumu ya kijeshi iwapo Ukraine itaendelea kuchelewesha mazungumzo ya amani.
Putin amesisitiza wakati wa upekuzi wa kituo cha Kamandi ya Vikosi vya Ulinzi vya Russia kwamba Moscow haitaruhusu Kiev ikwamishe mchakato wa amani.
“Ikiwa viongozi wa Kiev hawataki kusuluhisha suala hili kwa amani, tutakamilisha majukumu yote kupitia operesheni maalumu ya kijeshi,” amesema Rais Putin.
Rais wa Russia ameeleza kuwa viongozi wa Ukraine hawapigi hatua kuelekea kwenye ufumbuzi wa amani na kuongeza kusema: “Hilo tunalishuhudia hata leo hii, kwa bahati mbaya viongozi wa serikali ya Kiev hawana haraka ya kutatua mzozo huu kwa njia ya amani. Nilizungumzia suala hili mwaka mmoja uliopita katika hotuba yangu kwenye Wizara ya Mambo ya Nje.
Wakati huo huo makamanda wa vikosi vya majeshji ya Russia wamethibitisha kuwa nchi hiyo imeyadhibiti maeneo ya Rodynske na Artemivka katika jimbo la Donetsk na pia Huliaipole na Stepnohirsk huko Zaporizhzhia.
Mgogoro wa Ukraine ulioanza mwaka 2022 umefuatiwa na ya uingiliaji wa kisiasa na kijeshi wa nchi za Magharibi katika masuala ya ndani ya nchi hiyo, hatua ambayo Moscow inaaamini inayumbisha usalama katika maeneo ya karibu na mipaka ya Russia na kutishia usalama wa nchi hiyo.