Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergey Lavrov amesema kwamba, Moscow ingali inaunga mkono suuala la kuanzishwa kwa taifa huru la Palestina.

Sergey Lavrov amesema hayo katika mahojiano na TASS kuhusu matukio ya 2025 na kuongeza kuwa, “Russia inaendelea kutetea suluhu ya haki ya mgogoro kati ya Palestina na Israel na moja ya mambo muhimu katika suala hili ni kuanzishwa kwa taifa huru la Palestina lenye mamlaka kamili, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia.”

Lavrov amebainisha kuwa, “Haijalishi hali ndani na karibu na Gaza itatokeaje, tunasisitiza tena kujitolea kwetu kushinikiza kupatikana kwa suluhu ya haki ya mgogoro wa Palestina na Israel kwa msingi wa mfumo wa kisheria unaotambuliwa duniani.” 

Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Russia ameongeza kuwa, “Jambo kuu hapa ni kurekebisha dhuluma za kihistoria na kutoa nafasi ya kuanzisha kwa taifa la Palestina lenye uwezo na mamlaka.

Serikali ya Russia amekuwa ikisisitiza mara kwa mara juu ya udharura wa kuundwa kwa nchi huru ya Palestina mji mkuu wake ukiwa Quds tukufu.

Mara chungu nzima, Rais Vladimir Putin wa Russia amekuwa akitilia mkazo wajibu wa kutekelezwa maamizio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yanayosisitizia kuundwa nchi huru ya Palestina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *