Chanzo cha picha, Getty Images
Muda wa kusoma: Dakika 2
Chelsea na Leeds United ni miongoni mwa vilabu vya Ligi ya Premia vinavyomfuatilia kiungo wa kati wa Uingereza James McAtee mwenye umri wa miaka 23 katika klabu ya Nottingham Forest. (Mail)
Arsenal wanafikiria kumsajili beki wa AC Milan mwenye umri wa miaka 19 Davide Bartesaghi. (Caughtoffside)
Kiungo wa Roma na Ufaransa Manu Kone, 24, anatarajiwa kuhamia Manchester United msimu ujao. (Sportsmole)
Tottenham wako tayari kusalia na mlinzi wa Uholanzi Micky van de Ven, 24, kwa masharti sawa na beki wa kati wa Argentina na nahodha wa Spurs Cristian Romero, 27. (Teamtalk)
Beki wa Brighton na England Lewis Dunk, 34, amejitolea kusalia katika klabu hiyo kwa walau msimu mmoja zaidi baada ya kuongeza mkataba kulingana na idadi ya mechi. (Athletic – michango inahitajika)
Mshambuliaji wa Manchester United Joshua Zirkzee, 24, amehakikishiwa na kocha mkuu wa Roma Gian Piero Gasperini kwamba mshambuliaji huyo wa Uholanzi ana nafasi katika mfumo wake wa 3-4-2-1. (Gazzetta – kwa Kiitaliano)
Vilabu vya Nottingham Forest, Chelsea na Aston Villa vinamwinda mshambuliaji wa Bologna mwenye umri wa miaka 21 Santiago Castro. (Gazzetta dello Sport via Sport Witness)
Oxford United wanafikiria kumpa mlinzi wa zamani wa Chelsea John Terry kazi yake ya kwanza ya usimamizi. (Sun)