Tuzo mpya ya Mchezaji Bora wa Mechi (Man of the Match) imeanza kutolewa rasmi katika Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025, huku ikizidi kuwa gumzo kutokana na kupokelewa vyema kwa sifa za muundo wa kipekee iliyonayo ikielezwa inastahili kwa nyota wanaong’ara katika fainali hizo.

Kombe hilo jipya limekuwa likitolewa tangu mechi ya ufunguzi wa michuano hiyo inayoendelea huko Morocco siku nane zilizopita, likionyesha mabadiliko ya wazi katika namna ubora binafsi unavyotambuliwa kwa michuano hiyo mikubwa zaidi ya soka barani Afrika.

Kwa miaka mingi, tuzo ya Man of the Match ilikuwa haijabadilika sana, lakini katika AFCON 2025, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa kushirikiana na mdhamini mkuu TotalEnergies wamechagua kitu tofauti, kombe lililoundwa kuwakilisha umoja, utofauti na ukuaji wa hadhi ya soka la Afrika duniani.

Kombe hilo jipya linaundwa na miale 24 inayong’aa, kila mmoja ukiwakilisha moja ya mataifa 24 yanayoshiriki fainali za michuano hiyo kwa msimu huu wa 35 tangu kuasisiwa kwake mwaka 1957.

Mchanganyiko wa vifaa vilivyotumika unatofautisha kila taifa na jingine, huku namna mihimili hiyo inavyopinda na kuungana ikionyesha jinsi soka linavyowaunganisha watu, na kusherehekea nguvu na mchango wa kipekee wa kila taifa katika AFCON.

Katikati ya kombe hilo kuna ua la Damask Rose, ishara inayohusishwa na nchi mwenyeji wa michuano hiyo ya AFCON 2025, Morocco.

Ua hilo linaunda kitovu chenye mvuto mkubwa katikati ya kombe na hutumika kama kumbukumbu ya kuona ya mahali ambapo tuzo hiyo ilipatikana.

Tangu mashindano hayo yaanze, kombe hili tayari limetolewa kwa wachezaji waliocheza vyema zaidi katika kila mechi, akiwemo Brahim Díaz wa Morocco, ambaye alikuwa mpokeaji wa kwanza wa tuzo hiyo baada ya mechi ya ufunguzi ambapo taifa mwenyeji liliifunga Comoros mabao 2–0 mjini Rabat.

Hadi sasa washambuliaji wanaonekana kutawala tuzo hizo kuanzia zimetoka huku kipa mmoja tu akiwa ndiye kafanikiwa kuitwaa ambaye ni Mohamed Elshenawy wa timu ya Taifa ya Misri.

Waliotoa tuzo hadi sasa:

Ademola Lookman

Simon Msuva

Sadio Mané

Yohan Roche

Naël El Aynaoui

Youssouf Zaidou

Mohamed Elshenawy

Alfredo Ribeiro

Amad Diallo

Riyad Mahrez

Edmond Tapsoba

Elias Achouri

Nicholas Jackson –

Théo Bongonda

Omar Marmoush

Lyle Foster

Lassine Sinayoko

Brahim Díaz.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *